The House of Favourite Newspapers

KAPO YA MOBETO, TANASHA MJADALA KAMA WOTE!

Mwanamitindo Hamisa Mobeto akiwa na mpenzi wake.

LICHA ya kudaiwa kuwa ni bwana wa mtu lakini kapo ya Mwanamitindo Hamisa Mobeto na huyo mtu wa mtu wameibua gumzo la aina yake baada ya kushindanishwa na kapo ya Tanasha Dona na Nasibu Abdul ‘Diamond.

 

Mobeto alisababisha gumzo la aina yake wikiendi iliyopita baada ya kutupia picha akiwa na jamaa huyo ambaye jina lake halijanaswa vilivyo na kinasa sauti cha Udambwi, wakiwa wamevalia jezi za Klabu ya Simba siku klabu hiyo ilipokuwa inacheza na AS Vita ya Kongo DR.

Mitandaoni walichukua picha hiyo kwa kuipa herufi A na  kuifananisha na ya Tanasha akiwa na Diamond ambayo waliipa herufu B na ndipo mjadala uliposhika kasi. “A mwenzangu, hiyo nyingine haieleweki kama us*** wa ngomani hujui nani kajamba,” aliandika zuu_stylish2 huku wengine nao wakiunga mkono kapo ya Tanasha.

Comments are closed.