The House of Favourite Newspapers

Kapombe aweka rekodi ligi kuu

0

kapombe3-2.jpgMartha Mboma, Dar es Salaam

LICHA ya Ligi Kuu Bara kusimama, mpaka sasa katika orodha ya wafungaji wa ligi hiyo, Shomari Kapombe ni beki pekee ambaye amefunga mabao mengi na kuweza kuwafunika baadhi ya mastraika katika ligi hiyo huku wengi wakiwa hawana bao hata moja.

 Kapombe amefanikiwa kufunga mabao manne na kuwafunika mastraika kama Mussa Hassan ‘Mgosi’, Pape N’daw (wote Simba) ambao hawana bao hadi sasa, wengine ni kama Themi Felix (Mbeya City), Abasirim Chidiebere (Coastal Union) na wengineo.

Msimu wa mwaka 2013/14, Tumba Sued akiwa na Ashanti United alifanikiwa kuwa beki aliyefunga mabao matano akiwa beki pekee ambaye alifunga mabao mengi na kuweza kuwafunika baadhi ya washambuliaji mpaka ligi ilipokuwa inamalizika.

Mpaka sasa imechezwa michezo kumi huku wengine wakiwa wamecheza michezo tisa na tayari mabao jumla yaliyofungwa ni 144, ligi imesimama huku kinara wa mabao akiwa mshambuliaji wa Stand United , Elias Maguli mwenye mabao tisa.

Leave A Reply