Kapombe, Sakho Warejea Simba

WACHEZAJI waliokuwa wakisumbuliwa na majeraha kwenye kikosi cha Simba akiwemo Pape Ousmane Sakho na Shomary Kapombe, wameanza kurejea kwa kasi.

 

Kapombe aliumia kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United, huku Sakho akiumia mchezo wa pili dhidi ya Dodoma Jiji.

 

Jana katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Cambiasso, wachezaji hao walionekana kuwa fiti huku Kapombe akicheza mechi, Sakho akifanya mazoezi binafsi.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Gomes alisema: “Kwa upande wa wachezaji inafahamika kwamba wengi wanasumbuliwa na majeraha, lakini wapo ambao wameanza kurudi taratibu.

 

“Ukitazama kwa mfano Sakho, hayupo tayari sana kwa sasa. Kwenye eneo la mabeki hapo unaona kila mmoja anarudi kwenye uimara wake ukianza na Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Pascal Wawa na Kennedy Juma,” alisema Gomes.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam


Toa comment