Karatu Yasimama, Dkt, Slaa Atajwa Kutokushirikiana na Wananchi..
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) CPA. Amos Makalla, akiwa katika mkutano wake wa hadhara amesema kwa Sasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepoteza Dira ikiwemo Mvuto kwa Watanzania, hasa Kipindi hiki ambacho Taifa linajiandaa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Baadae mwaka huu.
Makalla ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wananchi kupitia kwenye Mkutano wa hadhara Wilayani Karatu mkoani Arusha.
“Hata Ninyi hapa si mnae Mzee Slaa ambae aliwahi kuwa Kiongozi wa Juu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), lakini hawezi kuja hapa kuwahamasisha kwa Sababu Chama hicho tayari kimepoteza Uelekeo” amesema CPA. Amos Makalla.
Akiwa katika mkutano wake wa hadhara wilayani Karatu alimwagiza Waziri wa Maji Jumaa Aweso kushughulikia kero ya maji ambpo waziri huyo tayari alisema amemuagiza Katibu Mkuu kupeleka Milioni Mia moja (100) Wilaya ya Karatu kwenda kukarabati Visima vilivyofukiwa na Mafuriko.
“Hapa Karatu Mjini tatizo kubwa ni Maji na nimeambiwa hasa baada ya Mafuriko kuna Visima vimefukiwa sasa shida hiyo isiwasumbue kwani tuna watekelezaji watakaolitatua kwa haraka jambo hilo na hapa tumpigie waziri wa Maji Mhe Aweso ajibu kuhusu suala hilo.
Mhe Juma Aweso alivyopigiwa simu amesema ” Ndugu Mwenezi wetu kwanza nakupongeza kwa kazi nzuri na suala hilo Mbunge wa Jimbo ameniambia na mimi namuuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji kuleta Milioni 100 ili kurekebisha miundombinu ya Visima vya Maji vilivyofukiwa na Mafuriko na Mimi mwenyewe nakuja uko mana tuna mradi wa Maji wa Bilioni nne ambao tutauanza katika Wilaya ya Karatu na uende ukamalize kabisa kero ya Maji”.