The House of Favourite Newspapers

KAREN: BABA NA PETIT MAN POA TU

Karen Gardner

MWANAMUZIKI anayechipukia kwenye Bongo Fleva, Karen Gardner ‘Malkia Karen’ amesema kuwa baba yake ambaye ni mtangazaji wa Radio Clouds FM, Gardner G Habash hana shida na meneja wa wasanii, Hemed Manungwi Petit Man kwa sababu anajua ukweli.  Karen aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, mitandao mingi ilikuwa ikiandika ndivyo sivyo kuwa yeye ana uhusiano wa kimapenzi na Petit Man, jambo ambalo si kweli.

Alisema familia yake inajua vizuri ishu hiyo kuwa ukaribu uliokuwepo kati yake na meneja huyo ni kwa ajili ya kazi. “Watu wengi ninaojuana nao na baba anajuana nao vizuri kwa hiyo hata hiyo habari ilivyoanza kuvuma haikuleta shida kwa sababu familia yangu inafahamu kila kitu kuhusu Petit Man,” alisema Karen ambaye anatamba na wimbo wake wa Washa. Hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii kulizuka tetesi kuwa mtoto wa huyo wa Gardner na Petiti Man ni wapenzi na walikuwa wakionekana sehemu mbalimbali wakiwa pamoja.

Comments are closed.