The House of Favourite Newspapers

Karia Aanika Pesa Zilizotumika TFF Tangu Awe Rais

RAIS wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia, ametaja matumizi ya fedha zilizotumika katika uendeshaji wa mashindano mbalimbali tangu aingie madarakani, Agosti 2017.

Akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari katika Hoteli ya SeaScape iliyopo Kunduchi, Dar es Salaam, Karia amesema tangu aingie madarakani, shirikisho limetumia jumla ya bilioni 3.7 katika uendeshaji wa soka Tanzania.

Fedha hizo zimegharamika kuendesha Ligi Kuu Bara, Kombe la FA mikoani pamoja na Kozi za Mafunzo mbalimbali yanayofanyika ndani ya TFF.

Aidha, Karia ameeleza kuwa TFF ilikuta deni kiasi cha shilingi bilioni 1.2 kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mfuko wa Jamii (NSSF), pia kutoka kwa wafanyakazi na watoa huduma mbalimbali ndani ya shirikisho, ambapo sasa madeni hayo yote yameshalipwa.

Vilevile Rais Karia, ameweka wazi kuhusiana na idadi ya wafanyakzi walio TFF kuwa ni 21, wakati awali walikuwa 41 na kupelekea kupunguzwa hadi kufikia idadi ya watu 21 huku wengi wao wakiwa wanajitolea.

Karia amesema wafanyakazi wengine wanafanya mafunzo kwa vitendo, na baadaye wanaweza kuajiriwa kama pale watakapoonekana uwezo wao ni mzuri.

 

Na George Mganga.

VIDEO: WADAU Misri Wafunguja Simba Ilivyoikimbiza Al Masry

Comments are closed.