The House of Favourite Newspapers

Karl Lagerfeld Afariki, Paka Atajwa Kurithi Utajiri Wake Bil 456

DIZAINA maarufu wa mavazi wa kampuni za Chanel na Fendi,  Karl Lagerfeld, amefariki jijini Paris, Ufaransa, baada ya kuugua kwa muda mfupi. 

Kifo chake kilichotokea jana (Jumanne) asubuhi, kimeombolezwa na watu maarufu katika tasnia ya mavazi, ikiwa ni pamoja na dizaina wa Italia, Donatella Versace.

“Leo dunia imempoteza mtu maarufu,” alisema mhariri mkuu wa jarida la Vogue, Anna Wintour.

Tovuti ya Lagerfeld inaonyesha alizaliwa mwaka 1938 japokuwa watu wengi wanasema alizaliwa miaka mitano kabla ya hapo.

Uvumi kuhusu kukumbwa kwake na ugonjwa, ulienea wiki kadhaa baada ya kutohudhuria maonyesho ya kampuni hiyo yaliyofanyika mwezi uliopita. Utaalam wake uliifanya Chanel kuwa moja ya makampuni maarufu ya kudizaini nguo duniani.

Watu maarufu wakiwemo Victoria Beckham, mwigizaji Kruger na mamodo Gigi na Bella Hadid waliomboleza kifo chake.  Pia mke wa Rais wa Marekani, Melania Trump, alishiriki maombolezo hayo katika mtandao wa Twitter akikumbushia dizaini aliyoifanya Lagerfeld alipozuru Ikulu ya White House kwa mara ya kwanza.

Imeelezwa kuwa, Paka aitwae Choupette aliyekuwa akimilikiwa na Karl Lagerfeld, ndiye anatazamiwa kurithi utajiri wa Mkongwe huyo anayetajwa kuwa na utajiri wa zaidi ya Tsh. Bilioni 456, Paka Choupette amekuwa akilelewa kifahari na Karl.

EXCLUSIVE: Mama GODZILLA Afunguka “MAKONDA Sio AKILI Yake”

Comments are closed.