The House of Favourite Newspapers

Karrueche ashangazwa kuimbwa na Chris

0

karrueche-tran (1)Karrueche Tran.

IKIWA imepita siku tatu tangu staa wa muziki wa Pop, Chris Brown kuachia albamu yake mpya ijulikanayo kama Royalty, mtangazaji maarufu, Karrueche Tran ‘Kae’ ameibuka na kuchukizwa na kitendo cha Chris kumuimba katika Wimbo wa Kae.

Katika wimbo huo wa Kae ambao upo katika albamu hiyo mpya ya Chris, umekuwa gumzo kwa mashabiki kutokana na Kae kuwahi kutoka kimapenzi na Chris.

chris-brown-shooting-at-concert__oPtChris Brown.

Kwa mujibu wa chanzo, Kae amechukizwa sana kuusikia wimbo huo ambao unasemekana kuna baadhi ya mistari amedisiwa.

“Karue ameusikiliza tena na tena, amechukizwa na baadhi ya maneno yaliyotumika japo ameamua kutulia lakini inaweza kuwa ugomvi mkubwa endapo Chris atajitokeza na kuupromoti wimbo huo mtaani,” kilisema chanzo.

Karue aliamua kutemana na Chris baada ya kugundua kuwa Chris alimsaliti kwa kutembea na mwanamke mwingine ambaye alizaa naye mtoto anayeitwa Royalty.

(Imeandaliwa na Andrew Carlos/ GPL)

Leave A Reply