The House of Favourite Newspapers

Kaseja Aachwa Kilimanjaro Stars, Aishi Manura Ndani

0

Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Juma Mgunda amemwacha kipa Juma Kaseja na kumchukua Aishi Manula katika kikosi chake cha wachezaji 22 watakaocheza mashindano ya Kombe la Chalenji Cecafa yatakayoaanza mwishoni mwa wiki hii.

 

Kilimanjaro Stars imeondoka leo Alhamisi ikiwa na matumaini ya kufanya vizuri katika Kundi B lenye timu za Kenya, Sudan na Zanzibar wakati Kundi A linaundwa na wenyeji Uganda, Burundi, Djibout, Eritrea, Somalia katika mashindano hayo.

Katika kikosi chake nahodha msaidizi Juma Kaseja ameachwa katika kikosi hicho na nafasi yake ikichukuliwa na kipa Manula.

 

Kaseja ameidakia Tanzania na kuisaidia kufuzu kwa CHAN2020, Cameroon pamoja na kufuzu kwa hatua ya makundi ya kusaka nafasi ya kucheza Kombe la Dunia 2022 Qatar.

 

Mgunda aliwahita Manula na Kaseja katika kikosi chake cha awali kilichokuwa na wachezaji 30, lakini leo katika kikosi cha mwisho jina la Kaseja halimo hiyo ni wazi ametoa nafasi kwa Manula.

Akizungumza wakati wa kutangaza kikosi hicho Mgunda alisema wachezaji wake wapo katika hali nzuri baada ya mazoezi ya leo asubuhi na watakaoachwa ni kutokana na sababu mbalimbali za kiafya na mambo mengine ya kiufundi.

Leave A Reply