The House of Favourite Newspapers

Kaseja apanda basi la Simba siku ya mechi

0

????????????????????????????????????

Kipa mkongwe nchini, Juma Kaseja.

Derick Lwasye, Mbeya

KIPA mkongwe nchini, Juma Kaseja, juzi Jumatano alijikuta akisababisha hali ya sintofahamu kwa mashabiki wa timu yake ya Mbeya City, hiyo ni baada ya kuingia ndani ya basi la Simba wakati wa mechi ya Tanzania Prisons na Simba kwenye Uwanja wa Sokoine.

Wakati mchezo huo ukianza, wachezaji wa Mbeya City walikuwepo uwanjani hapo kushuhudia kipute hicho cha Ligi Kuu Bara huku Kaseja akiwa ni mmoja wao, lakini ghafla kipa huyo alishuka na kuelekea kwenye basi la Simba ambalo ndani walikuwepo watu kadhaa akiwemo straika wa Simba, Hamis Kiiza.

Kaseja alibaki kwenye basi hilo la Simba kwa muda wote wa kipindi cha kwanza na baada ya dakika 45 akashuka na kurejea kwenye basi la Mbeya City kujumuika na wenzake.

Kitendo hicho kilipokewa kwa hisia tofauti na mashabiki walioshuhudia tukio hilo, hasa wale wa Mbeya City ambao hawakufurahishwa nacho hasa kwa kuwa katika mechi baina ya timu hizo, timu yao ilifungwa. Walisikika wakilalamika.

Leave A Reply