Kartra

Kaseke Aweka Rekodi Yake Yanga

NYOTA mzawa, Deus Kaseke anayecheza ndani ya kikosi cha Yanga ameweka rekodi yake ya kuwa mzawa anayefanya vema ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi.

 

Licha ya kutokuwa na zali la kupendwa na mashabiki wa timu hiyo, nyota huyo ni namba moja kwa wenye rekodi nzuri ndani ya Yanga kwa msimu huu wa 2020/21.

 

Amehusika kwenye jumla ya mabao 10 kati ya 43, yaliyofungwa na kikosi hicho ambapo amefunga mabao sita na ana jumla ya pasi nne za mabao.

 

Mbali na kuweza kufunga mabao hayo pia miguu yake iliamua timu hiyo kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya kufunga jumla ya mabao mawili kwenye mchezo wao dhidi ya Mwadui FC, uliochezwa Uwanja wa Kambarage.

 

Kwa upande wa nyota wa kigeni kinara wao ni Yacouba Songne ambaye ni namba moja kwa utupiaji akiwa na mabao 7 na ametengeneza pasi nne za mabao. Amehusika katika mabao 11 kati ya 43 yaliyofungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya pili na pointi 61.

Stori: Lunyamadzo Mlyuka,Dar es Salaam


Toa comment