Kashilillah Achukua Fomu ya U-Spika

 Aliyewahi kuwa Katibu wa Bunge hilo, Dk Thomas Kashilillah amejitosa kwenye kinyang’anyiro  cha uchukuaji fomu kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.

 

Dk Kashilillah alikuwa Katibu wa Bunge tangu mwaka 2009 hadi mwaka 2017 baada ya Hayati Rais John Magufuli kumhamisha nafasi hiyo na kumteua kuwa Naibu Katibu wa Wizara ya Kilimo, huku Stephen Kagaigai ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, akiteuliwa kushika nafasi hiyo.


Toa comment