The House of Favourite Newspapers

Kasi ya Magufuli ya kupunguza matumizi yawakuna wengi Afrika

rais magufuli

Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli.

Kutokana na kasi ya Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli hasa katika kupunguza matumizi ya serikali, watu wengi kutoka kona mbalimbali za Bara la Afrika wameonekana kumkubali kwa kutengeneza ‘Hashtag’ katika mtandao wa Twitter ya #WhatWouldMagufuliDo wakimaanisha kama angekuwa Magufuli angefanyaje.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Rais Magufuli kufuta sherehe za Uhuru na badala yake wananchi kuitumia siku hiyo kushiriki katika zoezi la kusafisha mazingira ili kupambana na ugonjwa wa kipundupindu nchini.

Rais Magufuli pia alipunguza bajeti ya hafla ya wabunge katika siku ya uzinduzi wa Bunge  kutoka milioni 225 mpaka milioni 24 na kuamuru fedha zilizobaki zipelekwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zikasaidie kununua vitanda.

Matumizi mengine aliyoyapunguza Rais Magufuli ni pamoja na kusitisha ziara za nje kwa viongozi wa serikali na kuzuia bajeti ya serikali kutumika katika kuandaa kadi za Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya na badala yake fedha hizo zisaidie kulipa madeni ya serikali.

Punguzo lingine alilolifanya Rais Magufuli ni la kufuta maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani na badala yake fedha za maadhimisho hayo zitumike kununua dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARVs).

Tangu Rais Magufuli aapishwe Novemba 9, 2015 zifuatazo ni baadhi ya meseji zinazosambaa katika mtandao wa Twitter zikionyesha kumkubali utendaji kazi wake wa kupunguza matumizi.

Credit: www.theguardian.com

Comments are closed.