Katavi: Aliyjenga Kituo cha Afya Avunja Madirisha ‘Sijalipwa’

MKANDARASI aliyefahamika kwa Borniface Exavery, aliyetengeneza madirisha ya Aluminium na kuyapachika katika Kituo cha Afya cha Katumba, amevunja madirisha hayo baada ya Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi, kumzungusha malipo yake, huku kazi akiwa amekwisha maliza muda mrefu.

 

Baada ya kutembelea eneo hilo, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera amedai mradi huo ulikuwa umekiuka taratibu mbalimbali za kisheria, ikiwemo upatikanaji wa tenda hiyo.

 

Aidha, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, ameeleza kushtushwa na hatua ya Mkandarasi huyo na kulitaka Jeshi la Polisi kumkamata huku akikiri Halmashauri kutomlipa malipo yake.

JPM: Usinilazimishe, Ombi Nimekataa – Video


Loading...

Toa comment