Kate Middleton: Nililazimika Kubadili Tabia Ili Nitoshe Katika Familia ya Kifalme
Kate Middleton, mke wa Prince William, mtoto wa King Charles III na mjukuu wa Hayati Malkia Elizabeth, amefunguka kuwa siku za mwanzo za maisha yake katika familia ya kifalme zilikuwa ngumu kwake ambapo alilazimika kubadilisha baadhi ya tabia zake ili kuendana na utamaduni wa familia hiyo.
Katika mahojiano maalum aliyoyafanya, Kate amesema miongoni mwa tabia ambazo alilazimika kubadilisha, ni tabia yake ya kupenda ‘kuchat’ muda mrefu na simu ambayo alikuwa nayo, ambayo hakuwa akijua kuwa haitakiwi kwenye familia hiyo, hasa wanapokuwa kwenye matukio ya wazi.
“Nililazimika pia kujifunza kutembea vizuri na namna ya kukaa hasa kwenye matukio ya kijamii. Nilijifunza kuwa pia haitakiwi kuzungumza na mtu mmoja kwa muda mrefu mnapokuwa kwenye mikusanyiko, kusalimiana na kila mtu kwa bashasha bila kujali mwonekano, hadhi au umri na mambo mengine mengi.
Kate amemshukuru Malkia Elizabeth na kueleza kuwa alikuwa mwalimu mzuri kwake kiasi cha kujenga ukaribu mkubwa kati yao.