Katibu Mkuu Chadema, Dkt. Mashinji Atimkia CCM – Video

ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Vicent Mashinji,  amekihama chama hicho na kujiunga Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Jumatatu, Februari 18, 2020, katika ofisi ndogo ya chama hicho Mtaa wa Lumumba Jijini Dar na kupokelewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole.

 

“Kilichonisukuma kuhamia CCM nii baada ya kutafakari mwenendo mzima wa siasa na uchumi nchini na kuangalia kina nani wako tayari, nikaona kwa upande wa Chadema bado huo utayari hatuna na tuko mbali sana katika kuchochea mambo ya maendeleo, tulikosa uelewa wa pamoja ndani ya chama na nje ya chama.

 

“Nikaona wenzetu wa Chama Cha Mapinduzi wanasikiliza, fursa ya kukaa tunalumbana asubuhi mpaka jioni nikaona inatuchelewesha, sasa tutaendelea siku gani?  Ninaona CCM iko tayari kuwaendeleza Watanzania na kule nilikotoka huu utayari bado sijauona.

 

“Tanzania haiumbwi na malaika bali binadamu na wanatofautiana, nimeona wenzetu wa CCM wanasikiliza sasa nikaona ni heri nije niongee na wenzangu nione kama nitapata fursa ya kutoa mchango kwa taifa langu.

 

“Miaka 47 bado ni kijana, kama Rais Magufuli anavyosisitiza maendeleo hayana chama hivyo nimuombe Mwenyekiti wa CCM kama ataridhia anikubalie nijiunge na chama hiki.”

TAZAMA TUKIO ZIMA HAPA


Loading...

Toa comment