Katibu Mkuu Dkt. Nchimbi Apokelewa Kwa Shangwe, Tayari Kuunguruma Mtwara




Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, leo amewasili Mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi ya siku tano.
Akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Masasi Katibu Mkuu Dkt. Nchimbi, amepokelewa na Viongozi wa Chama na Serikali na Vijana wa Hamasa.
Akisalimia mara baada ya kupokelewa Dkt.Nchimbi , amesema amefurahishwa na umoja waliouonyesha wanaccm wa Masasi Kwa namna walivyojitokeza Kwa wingi katika mapokezi.
Dkt.Nchimbi amesema waanamini Umoja na Utulivu wa nchi unategemea CCM kuendelea kuwa madhubuti.
Ameongeza kuwa CCM inaweza kuwa madhubuti kama wanaCCM wameshikamana, wanapendana, wanaahirikiana, wanatambua kama wanawajibu wa kuwatumikia watanzania Kwa nguvu zote na kama watachagua Viongozi wenye moyo wa kuwatumikia watanzania.
Ktika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa-NEC, Oganaizesheni, Issa Usi Haji Gavu, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA- Amos Makalla naKatibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa-SUKI- Rabia Hamid Abdalla.