Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Nchimbi Awasili Ethiopia kwa Ajili ya ziara ya Kikazi
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole Nchini Ethiopia leo Januari 31, 2025 na kupokelewa na Dkt. Girma Amente, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Prosperity Party (PP), Chama tawala cha Ethiopia na pia Waziri wa Kilimo wa Serikali ya nchi hiyo.
Balozi Nchimbi amewasili nchini Ethiopia kwa ajili ya ziara ya kikazi, kufuatia mwaliko wa PP.