Katibu Mwenezi CCM Kutikisa Kesho Diamond Jubilee

Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Mafunzo CPA. Amos Makalla kesho Jumamosi Julai 6,2024 ananasa ziara ya siku saba mkoani Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa na ofisi yake imesema kuwa komredi Amos Makalla ataanza ziara hiyo kwa kufanya mkutano wa ndani katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo pia atatambulishwa rasmi kuwa mlezi wa chama mkoa wa Dar es Salaam baada ya kuteuliwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Samia Suluhu Hassan wiki iliyopita katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC.