The House of Favourite Newspapers

Katibu wa CCM Wilaya ya Kilolo Auawa Kwa Kupigwa Risasi

Aliyekuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa, Bi Christina

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kupokea kwa mstuko mkubwa taarifa za kifo cha Katibu wa CCM Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa, Bi Christina
Kibiki aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiyojulikana.

Taarifa ya leo Novemba 13, 2024 iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Gabriel Makalla imebainisha kuwa Marehemu alikuwa anajiandaa kuhudhuria Semina elekezi kwa Makatibu Mjini Dodoma kesho.

“Chama Cha Mapinduzi kinatoa pole kwa familia, ndugu, viongozi na wanachama wa CCM Mkoa wa Iringa kufuatia kifo cha ghafla na cha kikatili.” imesema taarifa hiyo.

“Tunawaomba wanachama wetu wawe watulivu wakati vyombo vya dola vikifuatilia na kuchunguza tukio hili, ili wahusika waweze kufikishwa katika vyombo vya kisheria.”

FULL VIDEO: BONGE TARIMO AKITEKWA MCHANA KWEUPE DAR – APAMBANA HADI AKAJIOKOA – “TUTAKUFUATA”….