The House of Favourite Newspapers

Makalla: Teknolojia Inayotumika Kujenga Skuli za Zanzibar Ipelekwe Bara

Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu CPA Amos Makalla amesema Zanzibar kunajengwa shule au jina jingine Skuli nzuri za kisasa ambazo zinatumia gharama nafuu lakini zinatija kwani ni mfumo wa Ghorofa na zinajitosheleza kwa kila kitu

Mwenezi amesema hayo wakati akikagua Jengo la Skuli ya Kisasa Fuoni ambayo imejengwa kwa Chuma tu Mkoa wa Magharibi ikiwa ni Muendelezo wa ziara yake ya kichama Visiwani Zanzibar.

“Niwaombe waliojenga Skuli hizi za Ghorofa kwa teknolojia waende kule Bara mana kuna uhaba wa maeneo hivyo teknolojia hii itasaidia sana mfano hai mie nilipokuwa RC Dar es salaam na Mwanza shida kubwa ilikuwa ni maeneo hivyo inatahijika teknolojia kurahisisha kupata Miundombinu bora na safi kama hii ya hapa Zanzibar”

Aidha Mwenezi Makalla amepongeza Dkt Hussein Mwinyi kwa kutekeleza Ilani kwa vitendo.

“Ni teknolojia ambayo kwanza inapunguza gharama hivyo tumpongeze Dkt Hussein Mwinyi kwanza ameteleza Ilani kwa vitendo haya Maskuli anayojenga ni ya mfano kuanzia Pemba mpaka hapa Unguja na bado anawo mpango wa kujenga majengo kama haya Ishirini ni maendeleo makubwa sana”