The House of Favourite Newspapers

Katika Kuelekea Miaka 30 ya Huduma Tigo, Yaja na “Above Beyond” Wiki ya Huduma kwa Wateja

Afisa Mkuu wa Biashara Isack Nchunda (kushoto) Mkurugenzi wa Masoko Edwardina Mgendi (kulia), pamoja na wateja wetu waliokuwa nasi kwa miaka 30, wakifungua rasmi Wiki ya Huduma kwa Wateja 2024 kwa kukata utepe maalum. Tumeungana na Watanzania kwa miongo mitatu, tukijivunia kutoa huduma bora zaidi kote nchini.

Dar es Salaam, 7 Oktoba 2024: Ikiwa ni kuelekea wiki ya huduma kwa wateja Kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo imejipanga kuendelea kutoa huduma bora, za kibunifu, na kwa gharama nafuu kwa wateja wake wote.

Akizungumza mapema leo Afisa Biashara Mkuu wa kampuni hiyo, Isaack Nchunda, wakati wakiadhimisha wiki ya huduma kwa wateja alisema wanajitahidi kuhudumia wateja wao kwa namna ya kipekee.

“Timu yetu inahakikisha unapata thamani zaidi, kutoka kwenye huduma zetu za kama simu za mikopo kwa shilingi 650 kwa siku, hadi vifurushi vya saizi yako vinavyokidhi mahitaji yako.”

Fiber zinazokupa intaneti isiyo na kikomo, huduma zote hizi zimeboreshwa ili kuhakikisha wewe mteja unapata uzoefu bora zaidi.”

Amesema kampuni hiyo inajivunia mazingira mazuri ya biashara hapa nchini ambayo yanatoa fursa ya kutoa huduma bora kwa Watanzania.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo, Edwardina Mgendi, alisema Wiki ya Huduma kwa Wateja mwaka huu imejikita kuonyesha dhamira yao ya kuwapa wateja wake uzoefu wa kipekee katika kila hatua ya safari yao na Tigo.

Aidha katika Kitengo cha Masoko, Mgendi amesema kazi yao ni kuhakikisha kila bidhaa na huduma wanayoitoa kwa wateja wake inakidhi mahitaji yako ya kila siku, kwa ubunifu na ubora usio na kifani.

“Huduma zetu zinafikia viwango vya juu kwa wateja wetu – kutoka vifurushi vya simu vilivyobuniwa kwa ajili ya kila aina ya mtumiaji.”

“Tunafuraha kuwa mstari wa mbele katika kukuletea huduma zinazoendana na maisha yako, tukizingatia kila maoni na hitaji unalotoa.” Alimaliza kusema