KAULI YA DIAMOND BAADA YA UAMUZI WA MAHAKAMA – VIDEO

Diamond akiwasili mahakamani hapo.

 

KUFUATIA Mahakama ya watoto iliyo ndani ya Hakimu Mkazi Kisutu kuifuta kesi ya madai ya matunzo ya mtoto iliyofunguliwa na Hamisa Mobeto dhidi ya mwanamuziki Diamond Platinumz baada ya wawili hao kupatana, msanii huyo amefunguka kufurahishwa na uamuzi wa mahakama hiyo huku akisema kilichokuwa kikiendelea hapo awali kingeleta madhara hasa kuhusu suala la malezi ya mtoto huyo.

“Hii haikuwa kesi, bali tuliitwa kusuruhishwa na mahakama, hivyo tumeenda tukapatana, hapa tumekuja tena leo kwa ajili ya kuweka sawa kumbukumbu za mahakama ili isije ikatokea leo na kesho kikazungumzwa kitu kingine ambacho kitaleta shida.

 

“Ninawashauri wasanii wenzangu na wazazi kwa ujumla, jambo kama hili likitokea wasiweke majungu yao pamoja kwani watakayekuwa wanamtesa ni mtoto, badala yake waangalie namna bora ya kumsaidia mtoto wao,” alisema Diamond.

 

PICHA: DENIS MTIMA

 

 

KAULI YA DIAMOND BAADA YA UAMUZI WA MAHAKAMA

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment