Kauli ya Rais Kenyatta Mbele ya Rais Samia Kenya – Video

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Mei 05, ameanza ziara ya siku mbili nchini Kenya ambapo mbali na kufanya shughuli mbalimbali akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, lakini pia atalihutubia Bunge la Kenya.

 

HOTUBA FUPI YA KENYATTA IKULU YA NAIROBI

Leo hii tumepata nafasi ya kuongea na Rais Samia kuhusu mambo mbalimbali. Tumekubaliana kuimarisha uhusiano kati ya Nchi zetu na kutatua shida ndogondogo zinazowakumba wananchi wetu wanapofanya Biashara baina yao.

 

Hii ni safari ya kihistoria na inadhihirisha uhusiano wetu tangu tukiwa tunapigania Uhuru. Ni Safari ya kwanza kutembelewa na Rais Mama wa kwanza ktk Jumuiya yetu (EAC) kwahiyo tunakupongeza, na tunakupongeza kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM.

 

RTumeweka Mikataba kuhusu kujenga pipeline ya gesi toka #Mombasa hadi #Tanzania. Hii itasaidia kuhakikisha Viwanda na Nchi yetu vinapata energy ya kutosha. Pia tumeweka mkataba wa kuimarisha Culture and National Heritage, mkataba wa Utalii na Anga.

 

“Tumefanya mazungumzo na Rais Samia na tumewaelekeza Viongozi walio chini yetu kuondoa kero ndogondogo zinazowasumbua Wafanyabiashara na Wewekazaji wa Nchi zetu wanapotoka Nchi moja kwenda nchi nyingine.”

 

“Tuko na furaha tele kukukaribisha Rais Samia kwasababu tunakuona kama Dada yetu, tutaendelea kudumisha uhusiano mwema, Undugu na uchumi mwema wa Wananchi wa Kenya na Tanzania na Afrika Mashariki.”

 Tecno


Toa comment