The House of Favourite Newspapers

Kayira, Idd Seif waacha kazi BBC

0

              Aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji wa Uingereza BBC, Kassim Kayira.

vlcsnap-322919

Aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji wa Uingereza BBC, Idd Seif.
vlcsnap-323676

Kassim Kayira na Idd Seif wakiwa katika studio ya BBC.

vlcsnap-327856

vlcsnap-327492

Idd Seif na Kassim Kayira wakiagana.

vlcsnap-327568 vlcsnap-327929

Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji wa Uingereza BBC wakiwaaga watangazi hao.

Watangazaji bora kabisa wa Shirika la Utangazaji wa Uingereza BBC, katika kipindi cha Dira ya dunia, Kassim Kayira na Idd Seif wameacha kazi katika kituo hicho kikubwa duniani.

Kwa mujibu wa watangazaji hao wawili waliokuwa pamoja studio katika kipindi cha Dira ya Dunia kwa mara ya mwisho jana, walisema wameamua kuacha kazi na kurudi nyumbani Afrika ili kuendeleza miradi yao.

Idd Seif, ambaye alijiunga na BBC mwaka 1997 akitokea Kampala, Uganda, alisema ameamua kurejea Uganda ili aweze kusimamia miradi yake, baada ya kazi ya utangazaji kwa miaka 40. Alielezea huzuni yake kwa kuwaacha watu waliompokea vizuri na kufanya nao kazi kwa miaka 20.

Kwa upande wake, Salim Kayira, alisema alijiunga na shirika hilo akitokea kituo cha televisheni cha Rwanda miaka kumi iliyopita akiwa Mhariri. Alisema naye atarejea Afrika ambako atajishughulisha na kilimo pamoja na ufugaji na sehemu aliyoamua kuishi ni Uganda.

Watangazaji hao wameondoka miezi michache baada ya mtangazaji mwingine mahiri wa Kiswahili, Charles Hilary wa Tanzania kuacha kazi na kujiunga na kituo cha televisheni cha Azam. Taarifa ambazo hazijathibitishwa, zinasema wawili hao nao huenda wakajiunga na Azam tv.

 

Leave A Reply