The House of Favourite Newspapers

Kaze Adokeza Mikakati ya Usajili wa Yanga, Asema Hawawezi Kurudia Makosa Tena

0
Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze

KOCHA Msaidizi wa klabu ya Yanga raia wa Burundi Cedric Kaze amesema Yanga haiwezi kurudia makosa yaliyojitokeza mwanzoni mwa msimu ya kusajili wachezaji kisha kushindwa kupata kwa wakati vibali vya kufanyia kazi nchini (ITC).

 

Akiongea na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa Yanga dhidi ya Polisi Tanzania Kaze amebainisha kuwa viongozi wa klabu hiyo wanaendelea na jitihada za kuhakikisha wanakamilisha usajili wa wachezaji waliopendekezwa na benchi la ufundi kwa ajili ya kuimarisha kikosi hicho.

Kaze ametoa wito kwa mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa hapo kesho

Kwa upande mwingine Kaze amebainisha kuwa Nahodha wa klabu hiyo Bakari Mwamnyeto pamoja na mlinzi wa kulia Djuma Shaaban wana uwezekano mdogo wa kucheza pambano la kesho kutokana na kutopata muda mwingi wa kufanya mazoezi na timu lakini pia Djuma alipata majeraha katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union.

 

Kaze ametoa wito kwa mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wao dhidi ya Polisi Tanzania kwani utakuwa ni mchezo wa mwisho kwa Klabu hiyo kucheza jijini Dar es Salaam.

Leave A Reply