The House of Favourite Newspapers

Kaze Amkingia Kifua Michael Sarpong

0

CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga, amesema kuwa anaamini uwezo wa mshambuliaji wake, Michael Sarpong ni mkubwa lakini kwa sasa anakwama kufanya vitu vizuri kutokana na kukosa watu sahihi wa kumpa pasi za mwisho.

 

Ndani ya Ligi Kuu Bara, Sarpong raia wa Ghana, amefunga mabao manne kati ya 29 ambayo yamefungwa na timu hiyo inayoongoza Ligi ligi baada ya kucheza michezo 18.

Akizungumza na Spoti Xtra,Kaze alisema: “Kwa sasa anapitia kwenye kipindi kigumu kwa kuwa mashabiki wanapenda kumuona akifunga, lakini anashindwa kufunga kwa sababu hapati ile mipira mingi kutoka pembeni jambo ambalo tunalifanyia kazi.

 

“Baada ya muda atakuwa bora na atarejea kwenye ule ubora ambao mimi ninaufahamu kutoka kwake. Wakati unakuja na kila mtu atakubali uwezo wake.“Tatizo hilo nimeanza kulifanyia kazi kwa kutengeneza watu sahihi ambao watakuwa wanampa pasi kutoka pembeni.

Leave A Reply