The House of Favourite Newspapers

Kaze Amuingiza Rasmi Kikosini Kiungo Kinda

0

BAADA ya kuonesha kiwango kikubwa kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon, Benchi la Ufundi la Yanga linaloongozwa na Kocha Mkuu, Mrundi, Cedric Kaze limeahidi kumtumia kiungo Omary Rashidi ʻChibadaʼ katika michezo ya Ligi Kuu Bara na mashindano mengine msimu huu.

 

 

Chibada akitokea benchi, alicheza mchezo wake wa kwanza katika kikosi hicho ikiwa ni siku chache tangu apandishwe timu ya wakubwa akitokea U20.

 

 

Kaze alimpandisha kinda huyo hivi karibuni baada ya kumtazama kwenye mazoezi ya U20 yanayosimamiwa na kocha Said Maulid ambaye aliwahi kuichezea timu hiyo.

 

 

Kocha msaidizi wa timu hiyo, Juma Mwambusi, alisema kiwango alichoonyesha Chibada katika mchezo huo uliochezwa Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar, kimewapa sababu ya kumtumia zaidi kwenye kikosi chao cha kwanza.

 

 

Mwambusi alisema kuwa hiyo ni nafasi ya Chibada kuonesha kiwango kikubwa kila atakapopata nafasi ya kucheza katika kikosi ili amshawishi kocha Kaze amuingize katika kikosi cha kwanza.

 

 

“Chibada ni mchezaji mzuri anayeweza kuimudu vema nafasi ya kiungo anayoicheza hivi sasa, kwani ana uwezo mkubwa wa kuchezesha timu, kumiliki mpira, kupiga pasi zenye macho zitakazofi ka kwa wachezaji wenzake.

 

“Katika mchezo wake wa kwanza alioucheza dhidi ya African Lyon alicheza kwa dakika chache na kutuonesha kuwa ana kitu kizuri kwake, hivyo ni wakati wake yeye kumuonesha kocha Kaze ili aingie katika kikosi cha kwanza.

 

 

“Hadi tunampandisha kocha Kaze alikuwa amemuona kwenye mazoezi ya U20 na kuvutiwa naye kabla ya kumpandisha kikosi cha wakubwa ambaye hivi sasa yupo kambini,” alisema Mwambusi.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Leave A Reply