The House of Favourite Newspapers

Kaze Amvimbia Gomes wa Simba

0

BAADA ya Yanga kufanikiwa kutwaa kombe la Mapinduzi katika michuano iliyomalizika Januari 13, Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa anachoangalia kwa sasa ni kufanikisha timu yake hiyo kutwaa makombe yote msimu huu, likiwa pia ni lengo la kocha wa Simba Didier Gomes.

 

Yanga ambayo kwa misimu mitatu mfululizo imeshindwa kutwaa kombe la ligi kati ya msimu wa 2017/18, 2018/19 na 2019/20, ambapo misimu yote hiyo makombe yalitua kwa wapinzani wao Simba, kwa sasa imeonekana kuwa na uchu wa kutwaa makombe yote yanayoandaliwa hapa nchini.

 

Baada ya Kombe la Mapinduzi Yanga inawania Kombe la Ligi Kuu Bara ambapo kwa sasa wanaongoza msimamo wa ligi wakiwa na pointi 44, mbele ya Simba yenye pointi 35, wakipishana mechi tatu, pia inawania Kombe la FA ambalo na lenyewe msimu uliopita lilitua kwa wapinzani wao Simba.

Akizungumza na Championi Jumatano, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kwa sasa, timu yao hiyo chini ya kocha Kaze wamedhamiria kuhakikisha wanatwaa vikombe vyote vilivyo mbele yao baada ya la Mapinduzi hivyo kwa sasa wanahitaji Kombe la Ligi Kuu na FA.

 

“Moja ya mikakati ya Yanga chini ya kocha Kaze tuliyojiwekea msimu huu ni kuona tunafanikiwa kutwaa makombe yote, tumeanza la Mapinduzi sasa tunaliangalia la ligi kuu na Kombe la FA

“Kikosi chetu kipo vizuri tayari kipo Kigamboni kinaendelea na mazoezi katika kuhakikisha mwalimu anakiimarisha kikosi chake kabla ya mzunguko wa pili kuanza,tunatarajia kuwa na mechi ya kirafiki ili kumpa fursa mwalimu kujiandaa zaidi,” alisema Mwakalebela.

 

Huu ni kama mkwara kwa kocha wa Simba, Didier Gomes ambaye naye ameshasema kuwa anataka kuona anatawaa makombe yote anayowania.Gomes ambaye amejiunga na Simba hivi karibuni kwenye mkataba wake anatakiwa kuhakikisha kuwa anatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la FA.

STORI: KHADIJA MNGWAI, CHAMPIONI

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply