The House of Favourite Newspapers

Kaze Ataja Mbinu Pekee ya Ubingwa Yanga

0

BAADA ya kukaa kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Kocha Mkuu wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze, ameibuka na kuwaambia wachezaji kuwa kama wanataka kutimiza malengo yao ya kuchukua ubingwa, basi wasitoke katika nafasi hiyo ya kwanza waliyopo.

 

Kauli hiyo aliitoa baada ya kufanikiwa kuwatoa kileleni Azam FC waliopo nafasi ya pili wakiwa na pointi 26 na Yanga 31 wote wakicheza michezo sawa.

 

Katika michezo miwili iliyopita ya ligi waliyocheza dhidi ya Azam FC na ule na JKT Tanzania, Yanga kila mmoja ilipata ushindi wa bao 1-0, yaliyofungwa na Deus Kaseke.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Kaze alisema kuwa amefanya kikao na wachezaji wake mara baada ya mchezo dhidi ya JKT akiwataka kuendelea na kasi hiyo waliyoianza katika mzunguko wa kwanza kabla ya kwenda wa pili.

 

Kaze alisema katika siku saba zilizopita walikuwa na ratiba ngumu ya kucheza michezo mitatu mfululizo na kufanikiwa kupata pointi saba kati ya tisa ambazo siyo mbaya kwao kutokana na ugumu wa timu ambazo wamekutana nazo.

 

“Bado tunaendelea kuimarisha timu wachezaji wanapambana sana kuhakikisha timu inabaki kukaa kileleni, kwani malengo yetu ni kuendelea kuongoza hadi mwishoni mwa ligi, hii tu ndiyo mbinu inayoweza kutupa ubingwa.

 

“Michezo mitatu ndani ya siku saba hakuna mwili wa mchezaji unaweza kuhimili mchakamchaka huo, hivyo niwapongeze wachezaji wangu kwa kupambana kuhakikisha wanawapa furaha mashabiki wao.

Na Wilbert Molandi

 

Leave A Reply