The House of Favourite Newspapers

Kaze Awakomalia Mastaa Wake Yanga SC

0

KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amewataka wachezaji wake kuhakikisha wanaendeleza wimbi la kutopoteza mchezo katika mechi zote za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara ili kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa.

 

Yanga inaongoza katika Ligi Kuu Bara kwa kuwa na pointi 45 ikicheza michezo 19, huku wapinzani wao Simba wakiwa na pointi 39 wakicheza michezo 17 na kujikuta wakipishana pointi sita.

 

Taarifa ambazo Spoti Xtra imezipata kutoka Yanga, zinasema kuwa, kocha Kaze amewataka wachezaji wake kuhakikisha wanaendeleza mapambano kwa kujituma ili kutotoa nafasi kwa wapinzani wao kuwafikia.

“Yanga kwa sasa imejipanga kuhakikisha inafanikiwa kutwaa ubingwa msimu huu na ndiyo maana uongozi umeamua kufanya maboresho katika benchi la ufundi kwa kumleta mtaalamu wa viungo kutoka nje pamoja na kumteua kocha msaidizi mwenye kiwango kuhakikisha timu yetu inakuwa bora zaidi.

 

“Kocha Kaze amewataka wachezaji wake kuhakikisha hawatetereki hata kidogo licha ya matokeo ya sare dhidi ya Mbeya City na badala yake amewataka kuhakikisha wanajituma ili kuweza kufanikiwa kushinda mechi zote zilizo mbele yetu na kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu,” alisema mtoa taarifa huyo.

Stori: Khadija Mngwai, Dar

Leave A Reply