The House of Favourite Newspapers

Kaze: Siogopi Presha Yanga

0

 

WAKATI akiwa kwenye presha kubwa ya kibarua chake kuota nyasi kutokana na matokeo ambayo hayawafurahishi mabosi wake pamoja na mashabiki wa Yanga, Cedric Kaze amesema hana presha.

 

Kocha huyo wa Yanga ameweka wazi kuwa aliamua kuifundisha timu hiyo kubwa kwa kuwa anajua kwamba kuna changamoto kwenye kila timu jambo ambalo halimpi mashaka.

Kesho Kaze ana kazi ya kusaka ushindi mbele ya Coastal Union ambayo kwenye mchezo wa kwanza chini ya Kocha Mkuu, Zlatko Krmpotic ubao ulisoma Yanga 3-0 Coastal Union, Uwanja wa Mkapa.Akizungumza na Championi Jumatano alisema:

 

“Siogopi presha ndani ya Yanga, mimi ni mwalimu na ninatambua kwamba timu kubwa zina presha ndio maana nikakubali kusaini.

 

“Mashabiki wanahitaji kuona timu inapata matokeo ila haiwezi yote kuwa kwa haraka na pia najua kwamba wanahitaji kuona ninatwaa ubingwa hilo siwezi kuwaambia zaidi ya kuwataka waje uwanjani kushuhudia burudani,” alisema

Stori na Lunyamadzo Mlyuka na Ibrahim Mussa

Leave A Reply