Kazi Imeanza …Yondani, Bocco Wawekewa Bilioni Mezani

John Bocco

TAIFA Stars yenye mastaa kama Kelvin Yondani, Erasto Nyoni, Fei Toto na John Bocco ina uhakika wa Sh. Bilioni 1.4 kwa kitendo cha kufuzu fainali za Afrika mwaka huu.

 

Stars chini ya nahodha na mchezaji tajiri zaidi Tanzania, Mbwana Samatta, ilifuzu fainali hizo zinazochezwa Misri kuanzia Juni 21 mpaka Julai 19 na ipo Kundi C na Kenya, Senegal na Algeria.

 

Kwa mujibu wa Caf, kama Stars itabeba ubingwa michuano hiyo itapata Sh.Bil. 10.3, lakini hata Stars ikienda kutalii Misri kwa maana ya kupoteza mechi zote bado ina uhakika wa Sh.Bilioni 1.4 ambazo hazina mjadala kwenye michuano hiyo yenye nchi 24 msimu huu.

Rais wa Caf, Ahmad Ahmad ameliambia Spoti Xtra kwamba zawadi za safari hii zimeboreshwa na wanatarajia yatakuwa mashindano ya aina yake.

 

“Tumeongeza fedha za washindi kwenye mashindano ya msimu huu,” alisema Ahmad akizungumzia mashindano hayo ambayo Stars wameyapania.

Mabingwa watetezi Cameroon msimu uliopita walipata Sh.Bilioni 9.2 na mshindi wa pili ambaye Misri akaambulia nusu yake. Zawadi zipo mpaka kwa mshindi wa nne. Mechi ya kwanza Stars itacheza na Senegal.

STORI NA MWANDISHI WETU, SPOTI XTRA, APRILI 18, 2019


Loading...

Toa comment