The House of Favourite Newspapers

Kcee amzawadia mama yake gari kama zawadi ya ‘birthday’

0

dsc_6200Staa wa muziki kutoka Nigeria, KCEE a.k.a Limpopo Master.

STAA wa muziki kutoka Nigeria, KCEE a.k.a Limpopo Master juzi kati alifanya kufuru baada ya kuzawadia mama yake ‘ndinga’ mpya aina ya Land Cruiser Prado.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, KCEE alitupia picha ya maza wake pamoja na ndinga hiyo kisha akaambatanisha maneno yaliyosomeka;

“Mpendwa mama yangu, kama ningelikuwa na njia yangu pekee ningenunua dunia nzima kwa ajili yako itambue kuwa wewe kwangu ni zaidi ya malaika. Asante sana kwa kuniamini hata pale wengine walikuwa hawaniamini, naheshimu sana unavyonijali na kunipa sapoti katika kazi zangu. Kwa mara ya kwanza nikutakie heri ya kuzaliwa St.

om, kamanda wangu nimekupatia mkoko mpya ndani ya nyumba yako. Heri tena ya kuzaliwa mama wa KCEE LIMPOPO.”

Leave A Reply