The House of Favourite Newspapers

Kcee awatumia mashabiki vocha zilizotumika!

0

kcee1Mwanamuziki wa matawi ya juu nchini Nigeria, Kcee.

KATIKA kila kinachosemekana kutafuta umaarufu zaidi au kitendo cha bahati mbaya, mwanamuziki wa matawi ya juu nchini Nigeria, Kcee, alijikuta akishambuliwa na mashabiki wake mwanzoni  mwa mwaka mpya (2016) wakisema aliwatumia vocha za simu ambazo zilikuwa tayari zimetumika.

Januari 5 mwaka huu, mwimbaji huyo alianza kuwarushia namba za vocha mashabiki wake, namba ambazo tayari alikuwa amewarushia mashabiki wengine na baada ya kuziingiza kwenye simu zao, walikuta zikigoma kutumika.

Mashabiki hao walianza kumshambulia mwimbaji huyo aliyedai alikuwa hafahamu kwamba kadi hizo alikuwa amezituma pia kwa mashabiki wengine.

“Jamani,  samahani kwa kuchanganya mambo, sikufahamu kwamba kadi hizo nilikwishazituma kwa watu wengine jana.  Asanteni kwa kulitambua hilo.  Hizi ni kadi za mwisho kwa leo, nitazichambua zilizobakia na kesho tutaendelea.  Asanteni,” aliandika kwenye mtandao wake wa Instagram.

Leave A Reply