KEISHA: NINAMUDU MUZIKI NA SIASA

Tokeo la picha la Khadija Shaban Taya ‘Keisha’

Khadija Shaban Taya ‘Keisha’

MWANAMAMA mkongwe kwenye gemu la Bongo Fleva, Khadija Shaban Taya ‘Keisha’ amefunguka kuwa kuna ugumu wa kufanya muziki na siasa ingawa kwa upande wake anamudu vyote kwa pamoja.

 

Akipiga stori na Risasi Vibes, Keisha ambaye anatarajia kuachia video ya ngoma yake mpya ya Nioe alieleza kuwa, muziki na siasa ni kazi ambazo kwa upande fulani zinaen-dana kwa sababu unafa-nya kwa ajili ya watu amba-po kwen-ye muziki ni mashabiki na kwenye siasa ni wananchi ambao wanahitaji uwawakilishe na kutatua matatizo yao.

 

“Ukiwa kwenye muziki unatakiwa kuwa na ubunifu, kujitoa na kujituma ndiyo vitu vya msingi ambavyo hata kwenye siasa vitu hivyo vinahitajika kwa kiasi kikubwa. “Kwa hiyo kuna ugumu fulani kufanya vitu hivi kwa pamoja, lakini ukiwa na moyo wa kufanya kama mimi, ni lazima utavimudu,” alisema Keisha ambaye kwenye siasa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC).


Loading...

Toa comment