Kenya: Mchekeshaji wa Miaka 19 Apewa Mkataba na Rihanna

Mchekeshaji Elsa Majimbo ambaye amejipatia umaarufu kwa hotuba zake katika mtandao wa Twitter na Instagram tangu kuanza kwa mlipuko wa Corona, amefanikiwa kuingia mkataba na nembo ya fasheni ya Rihanna kwa jina Fenty.

Mchekeshaji huyo mwenye umri wa miaka 19 alisema kwamba anajivunia mkataba wake wa kukuza nembo hiyo ya Rihanna. Nembo hiyo ya Rihanna ilituma ujumbe kwa njia ya video katika mtandao wa twitter ambapo ilitangaza mpango huo.
Toa comment