The House of Favourite Newspapers

Kenya yarahisisha masharti ya safari kwa nchi za Afrika

Kenya imetangaza kuwa, itawaruhusu raia wa karibu mataifa yote ya Afrika kutembelea nchini humo bila kuhitaji idhini ya awali (visa). Hiyo ni kwamujibu wa agizo jipya la baraza la mawaziri la nchi hiyo.

Kuanzishwa kwa Idhini ya Usafiri wa Kielektroniki (ETA), ambayo ilichukua nafasi ya hitaji la visa kwa wageni wote, ilikosolewa na wakosoaji wakasema ni kama visa chini ya jina lingine.

Jana Jumanne Januari 21, 2025, taarifa ya baraza la mawaziri ilisema ETA itaondolewa kwa nchi zote za Afrika isipokuwa Somalia na Libya – kutokana na sababu za kiusalama.

Taarifa ya serikali ya Kenya ilisema, hii ni sehemu ya juhudi za kuunga mkono sera za wazi na ukuaji wa utalii na kukuza ushirikiano wa kikanda sambamba na kurahisisha usafiri katika bara zima. Hatua hiyo inalenga kuboresha sekta ya utalii.

Mwaka jana, Kenya ilianzisha sera ya “bila visa” ambayo ilihitaji wageni wengi kutuma maombi mtandaoni ili kupata idhini kabla ya kuondoka nchini mwao.

MABODIGADI WALIVYOZUNGUKA GARI la RAIS MWINYI na MKEWE WAKISHUKA na KUPANDA GARI LINGINE BARABARANI