The House of Favourite Newspapers

Kerr avuruga kikosi Simba

0

Mohammed Mdose, Dar es Salaam

HAKUNA kukariri kuhusu kikosi cha kwanza cha Simba na kocha wa timu hiyo, Dylan Kerr, amesema siyo lazima katika beki ya kati wacheze Juuko Murshid na Hassan Isihaka kwani kuna vifaa vingine hatari.

Katika mechi tisa za Ligi Kuu Bara zilizopita, Simba ilionekana ikiwatumia mabeki hao kiasi cha kuonekana kama ni nafasi zao za kudumu kikosini.

Kerr ambaye timu yake ipo kambini Zanzibar kujiandaa na mechi dhidi ya Azam FC, Desemba 12, mwaka huu, alisema hakuna mchezaji aliyejihakikishia nafasi katika kikosi chake na muda wowote kinaweza kubadilika.

 “Huenda wale waliokuwa wakionekana zamani wasionekane katika mechi zijazo, nataka kuwe na ushindani ili kila mchezaji acheze kwa kujituma zaidi.

“Simba ina mabeki wengi wa kati ambao watacheza kwa umahiri mkubwa sana kama wakitambua hilo, nitamtumia yeyote ambaye ataonyesha uwezo mzuri.

“Yupo Isihaka, Juuko, pia kuna huyu chipukizi anaitwa Said Issa naye ni mzuri, Justice Majabvi, Abdi Banda nao wanaweza kucheza vizuri nafasi hiyo, hivyo atakayefanya vizuri mazoezini ndiye atakayecheza,” alisema Kerr.

Leave A Reply