The House of Favourite Newspapers

Kerr: Kiiza amekuwa mtamu

0

IMG_2238

Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr.

Musa Mateja na Martha Mboma
SIKU saba kabla ya Simba kukutana na Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara, Simba imeanza tambo ambazo zinaonyesha kuwa wana uhakika wa kupata ushindi kwa kiwango cha juu.

Simba imeanza tambo hizo zikiwa ni siku chache baada ya kupata ushindi mfululizo katika mechi mbili za ligi hiyo jijini Tanga, ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema Yanga wajiandae kwa kipigo na kama hawaamini basi wasubiri supu ya mawe inakuja.

Wakati Hans Poppe akisema hayo, Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr, ametambia ubora wa mshambuliaji wake, Hamis Kiiza katika kufunga mabao unaowanyamazisha wale wote waliokuwa wakimkosoa mchezaji huyo.

Kerr amesema hayo mara baada ya Kiiza kufunga mabao mawili katika mechi hizo dhidi ya African Sports na ile ya Mgambo ambapo ameiwezesha timu hiyo kufikisha pointi sita, sawa na Yanga ambayo wanatarajiwa kukutana nao Jumamosi ijayo.

“Nawashangaa sana wale ambao walikuwa wanamhukumu na kumbeza Kiiza kuwa hafungi lakini kwa sasa ameanza kuonyesha uwezo wake na hata kuwaumbua waliokuwa wakimsema vibaya na watambue ndiyo ameanza kazi.

“Walisema Simba haina mastraika hasa kipindi cha ‘pre seasons’, kitu ambacho si kweli, nina wachezaji wazuri, zaidi ninahitaji kuwajenga wawe bora zaidi hata kuweza kuisaidia timu, hasa kufunga mabao mengi.

“Ndiyo maana napambana na Kiiza, nimempa jukumu la kufunga mabao 20 wakati mastraika wengi wao watafunga mabao kuanzia 10 kwenda juu,” alisema Kerr.

Gazeti hili lilipomuuliza Hans Poppe juu ya mwenendo wa timu yao na maandalizi ya mechi zao zijazo, alisema: “Kwanza timu bado ipo Tanga, itarejea Dar kesho (leo) lakini tumefurahishwa na matokeo, kikosi chetu kipo vizuri, Yanga wasubiri supu ya mawe tu waone utamu wake.”

Leave A Reply