The House of Favourite Newspapers

KESHO BONGE LA COMEDY, NYERERE, JK, MC PILIPILI, BLACK PASS NDANI

Oscar Nyerere akiongea na Global TV.

Kiongozi wa Kundi la Chekelea Stand Up Comedy, Oscar Luambano a.k.a Oscar Nyerere akizungumza na wanahabari kwenye Hoteli ya Kebbys iliyopo Mwenge jijini Dar, amesema kundi hilo kesho linatarajia kufanya tamasha kubwa kwenye ukumbi wa hoteli hiyo.

Dogo Pepe amesema kesho atafanya ambavyo hajawahi kufanya na kuwavunja mbavu watakaohudhuria.

 

Oscar amewataja baadhi ya wachekeshaji wenzake atakaokuwa nao katika tamasha hilo kuwa ni pamoja na MC Pilipili, Dogo Pepe, Back Pass, JK Comedian na wengineo.

 

Back Pass akisalimiana na jamaa anayefagilia sana swaga zake.

Katika tamasha hilo, mgenio Rasmi anatarajiwa kuwa ni Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michgezo, Juliana Shonza huku waimbaji wa Injili akiwemo Emmanuel Mbasha na mastaa wengine wa filamu wakitarajiwa kutinga ndani.

 

Mapaparazi wakimuhoji mmoja wa wasanii wa kundi hilo.

 

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL

Chekelea Stand Up Comedy Kufanya TAMASHA Kubwa La Vichekesho Kesho

Comments are closed.