The House of Favourite Newspapers

Kesi ya Bomoabomoa Dar yawakusanya waathirika mahakamani

0

1.Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar waliobomolewa nyumba zao zilizokuwa mabondeni wakiwa nje ya Mahakama ya Ardhi jijini Dar. Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar waliobomolewa nyumba zao zilizokuwa mabondeni wakiwa nje ya Mahakama Kuu ya Ardhi jijini Dar.2.Baadhi yao wakionekana kutafakari kujua hatima ya kesi hiyo itakavyokuwa.Baadhi yao wakionekana kutafakari ili kujua hatima ya kesi hiyo.

3.Wakazi  wanaodaiwa kubomolewa nyumba zao za mabondeni wakiwa wamekaa nje ya Maduka yaliyopo eneo la Mahakama hiyo.Wakazi  wanaodaiwa kubomolewa nyumba zao za mabondeni wakiwa wamekaa nje ya Maduka yaliyopo karibu na eneo la mahakama hiyo.

KESI ya kupinga bomoabomoa iliyofunguliwa na Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia (CUF) katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi jijini Dar es salaam imeunguruma tena leo ambapo baadhi ya wakazi waliobomolewa nyumba walionekana kukusanyika nje ya mahakama hiyo.

Kesi hiyo namba 822 ya mwaka 2015 inasikilizwa na Jaji Penterine  Kente huku upande wa walalamikaji wakisimamiwa na wakili Abubakar Salim.

Kamera yetu ya mtandao huu wa Gpl ilifika mahakamani hapo leo asubuhi  na kukuta wananchi hao wakiwa nje ya mahakama hiyo na ilikuwa bado haijaanza kusikilizwa muda wa saa tano asubuhi. Wananchi hao walijikusanya nje kama picha zinavyoonesha.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply