The House of Favourite Newspapers

Kesi ya Gachagua kusikilizwa leo

Mapema kuanzia saa tano japo la majaji liliteuliwa na Mahakama kuu nchini Kenya, Limeanza kusikiliza kesi ya kuondolewa madarakani Kwa Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua, ikiwa ni siku chache baada ya tamko la mahakama hiyo kutaka mabadiliko hayo yasitishwe ikiomba kupitia Kwa makini kesi hiyo.

Gachagua ambaye aliondolewa mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya seneti kupiga kura, ambapo idadi ya kura zilifikia theluthi na kufanya kuondolewa, huku nafasi yake kuchukuliwa na Kithure Kindiki aliyeteuliwa na Rais William Ruto na kupitishwa Kwa asilimia 100 ya kura za bunge la seneti nchini humo.

Gachagua ambaye alituhumiwa Kwa makosa kadhaa ikiwemo, kuhamasisha ukabila na kukiuka misingi ya kikatiba, alishindwa kuhudhuria katika bunge la seneti wiki iliyopita baada ya kupata changamoto za kiafya, huku baadaye aliiomba mahakama kuliamuru bunge kufuta taarifa za uongo dhidi yake, akidai hazina ushahidi wa kutosha.

Katika hatua nyingine Wafanyakazi walio chini ya Naibu Rais aliyeshtakiwa, Rigathi Gachagua, wamezuiwa kuingia katika jengo la Harambee House, Nairobi, siku chache baada ya kupewa likizo ya lazima. Kulingana na ripoti, maafisa kutoka Kikosi cha Rapid Deployment Unit (RDU) walikuwa wamepiga kambi nje ya jengo hilo Jumanne na kuwazuia wafanyakazi wote walioripoti kazini.