The House of Favourite Newspapers
gunners X

KESI YA KINA RUGEMALIRAYAAHIRISHWA HADI DESEMBA 8

0
James Rugemalira (aliyepunga mkono kushoto) na Harbinder Singh wakitoka katika mahakama ya Kisutu katika moja ya matukio ambapo kesi yao ilisikilizwa.

 

KESI ya James Rugemalira na Harbinder Sing Sethi imeahirishwa hadi  Desemba 8 mwaka huu kutokana na upelelezi kutokamilika.

 

Kesi hiyo inasikilizwa na Mahakama ya Mkazi Kisutu na Hakimu Mkazi, Huruma Shaidi.

 

Wakati huohuo, upande wa utetezi umemueleza hakimu kuwa unaomba upelelezi ukamilike kwa haraka kwa sababu hali ya mshtakiwa (Sethi) si nzuri.

 

Upande wa Jamhuri nao umedai kuwa unafahamu kuwa washtakiwa wana haki zao na ndiyo maana wanajitahidi kukamilisha upelelezi kwa wakati muafaka.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply