The House of Favourite Newspapers

Kesi ya mita 200 yaahirishwa tena

0

3.Dk. akifanya mahojiano na wanahabri.Wakili wa serikali Dk.Tulia Ackson akifanya mahojiano na wanahabari jana.

4.Wakili Peter Kibatala wa upande wa mlalamikaji akitoka katika chumba cha mahakama kwenye kesi hiyo hapo jana.

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania leo imehairisha tena kesi namba 37 ya mwaka huu, ya mlalamikaji kuiomba mahakama itoe tafsiri ya kifungu cha 104 kidogo cha (1) cha Sheria ya Uchaguzi kama kinazuia ama la wananchi kukaa umbali wa mita 200 baada ya kupiga kura katika vituo.

Kesi hiyo sasa itatolewa maamuzi maalum kesho saa 4 asubuhi.

Katika kesi hiyo, mawakili wa serikali wanaongozwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali, Dk.Tulia Ackson huku upande wa mlalamikaji ukiongozwa na Peter Kibatala.

Shauri hilo lililofunguliwa na Mgombea Ubunge Viti Maalumu Jimbo la Kilombero (Chadema), Amy Kibatala, akitaka mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya kifungu cha 104 (1) cha Sheria ya Uchaguzi.

Leave A Reply