The House of Favourite Newspapers

Kesi ya Mke wa Bilionea Msuya Yaahirishwa Hadi Mwaka Kesho

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeahirisha kesi ya mauaji inayomkabili mke wa bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrina na mwenzake baada ya upande wa mashtaka kueleza kuwa upelelezi haujakamilka.

 

Wakili wa serikali, Patrick Mwita, amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wa kesi haujakamilika na baada ya kueleza hayo hakimu ameiahirisha kesi hiyo hadi Januari 8 mwaka kesho.

 

Mbali ya mshitakiwa huyo, mwingine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara, Revocatus Muyella ambaye kwa pamoja na Mrina wanakabiliwa na kesi ya mauaji namba 5 ya mwaka 2017.

 

Watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kumuuwa dada wa marehemu bilionea Erasto Msuya aitwaye, Anathe Msuya huko Kigamboni.

Comments are closed.