The House of Favourite Newspapers

Kesi ya Mo Dewji Kutekwa Ilipofikia

UPANDE  wa Jamhuri katika kesi inayomkabili dereva wa teksi mkazi wa Tegeta, Mousa Twaleb (46),  ya uhujumu uchumi ikiwamo kusaidia kutendeka uhalifu, kutakatisha Sh. milioni nane na kumteka Mohamed Dewji maarufu kama ‘Mo’ umedai kuwa bado unaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine wanne kwa ajili yakuwaunganisha katika kesi hiyo.

 

Kesi hiyo ilitajwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

 

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, amedai kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, na kwamba bado upande wa Jamhuri unaendelea na juhudi za kuwatafuta watuhumiwa wengine.

 

Alidai kuwa upande wa Jamhuri unaomba tarehe nyingine ya kutajwa na hakimu amesema kesi hiyo itatajwa tena Septemba 30, mwaka huu na mshtakiwa ataendelea kukaa mahabusu.

Comments are closed.