The House of Favourite Newspapers

Kesi ya Shehe Mpemba Kinara wa Meno ya Tembo Aliyetajwa na Rais Magufuli Yapigwa Kalenda

shehe-mpemba-wa-meno-ya-tembo-8

DAR ES SALAAM: KESI inayomkabili mtuhumiwa wa makosa ya kukamatwa na nyara za serikali, Yusuf Ali Yusuf maarufu kama Shehe Mpemba (35)  ambaye alitajwa na Rais John Magufuli kuwa ndiye kinara wa biashara ya meno ya tembo, leo Desemba 1, 2016 imeahirishwa hadi Desemba 15 kufuatia kutokukamilika kwa upelezi wa kesi hiyo.

Akitaja kesi hiyo, Wakili wa Serikali katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Thomas Simba amewasilisha hoja kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika ambapo Hakimu Simba aliamua kuipanga kesi hiyo isikilizwe tena Desemba 15 mwaka huu na kumtaka wakili huyo akamilishe haraka upelelezi ili kesi hiyo isikilizwe na kutolewa maamuzi.

Turudi nyuma

Mpemba na wenzake watano, wanakabiliwa na mashitaka manne ya kula njama za kufanya uhalifu na kukutwa na nyara za serikali kinyume na sheria.

Akisoma mashtaka hayo, Novemba, 16 mwaka huu, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Paul Kadushi,  alisema kwa nyakati tofauti kati ya Januari 2014 na Oktoba 2016, jijini Dar es Salaam, Morogoro, Iringa, Tanga na Mtwara, watuhumiwa hao walitenda makosa hayo.

Mtuhumiwa huyo na wenzake Charles Mrutu (37), Benedict Kungwa (40), Jumanne Chima (30), Ahmed Nyagongo (33) na Pius Kulagwa (46)  hawakutakiwa kujibu chochote na kesi hiyo iliahirishwa hadi Desemba Mosi (leo), na watuhumiwa hao walirudishwa rumande.

Mwezi Oktoba mwaka huu, Rais Magufuli alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii jijini hapa, alimtaja Mpemba kwamba amekuwa akisikia habari zake kwenye taarifa za kuhusika na biashara hiyo haramu na kuwapongeza waliofanikisha kukamatwa kwake.

halotel-strip-1-1

Comments are closed.