Kesi ya R. Kelly juu ya unyanyasaji wa kingono yaibuka upya

 

WANAWAKE wengine wawili wamejitokeza na madai ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya mwanamuziki wa R&B,R Kelly.

 

Rochelle Washington na Latresa Scaff walizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuwa walipewa kinywaji pamoja na madawa ya kulevya mara baada ya tamasha la mwanamuziki huyo lililofanyika Baltimore miaka ya 1990.

 

Wanawake hao walisema kuwa mwanamuziki huyo aliwapeleka katika chumba cha hoteli bila ridhaa yao na kutaka kufanya nao mapenzi.

 

Kelly mwenye umri wa miaka 52, amekuwa akishutumiwa kwa madai ya unyanyasaji wa kingono kwa wanawake kwa miongo kadhaa lakini hakuwahi kukamatwa wala kukiri makosa yake.

 

 

Wakizungumza na waandishi wa habari, wamesema kuwa wakati huo ambao Kelly aliwachukua kwenda kwenye tamasha walikuwa vijana wadogo.  Vilevile walishindwa kusema ni mwaka gani sahihi ambao walinyanyaswa kingono bali walisema ni kati ya mwaka 1995 au 1996.

 

Bi Scaff mwenye umri wa miaka 40, anasema kuwa katika sherehe hiyo ya muziki walipewa madawa ya kulevya aina ya ‘cocaine’, bangi na pombe na kualikwa kumsubiri mwanamuziki katika chumba cha hoteli. Wakiwa katika chumba hicho, waliambiwa wavue nguo kwa sababu Kelly alikuwa karibu anafika.

 

Mwanamuziki huyo alifika akiwa ameacha sehemu yake ya siri wazi, Bi. Scaff amesema mwanamuziki huyo aliwataka wafanye mapenzi wakiwa watatu kwa pamoja.

 

Bi Washington ambaye sasa ana umri wa miaka 39 alikataa na kwenda bafuni wakati ambapo Scaff alibaki na kufanya naye mapenzi ingawa si kwa ridhaa yake, ni kwa sababu ya kulewa pombe na madawa ya kulevya, alisimulia.

 

 

Scaff alisema kuwa ameamua kuliweka jambo hilo wazi kwa sababu wao ni waathirika kama waathirika wengine wa ngono.

 

Wanawake hao wawili waliwakilishwa na wakili mashuhuri Gloria Allred na pia aliwawakilisha wanawake wengine ambao walitoa malalamiko yao dhidi ya Kelly.

 

Akituma ujumbe kwa mwanamuziki huyo maarufu duniani Scaff alisema: ” Huna pa kukimbilia au kujificha. Umeweza kukana makosa yako maovu kwa muda mrefu.”

 

R Kelly ambaye jina lake halisi ni Robert Sylvester Kelly, amekutana na shutuma za unyanyasaji wa kingono kwa miaka zaidi ya ishirini.

 

Katika makala ya hivi karibuni inayoitwa , ‘Surviving R Kelly’, ambayo ilikuwa inaonyeshwa katika chaneli moja ya televisheni inayoitwa ‘Lifetime’, imeeleza namna ambavyo amefafanua madai yake dhidi ya unyanyasaji wa kingono kwa wanawake. Hata hivyo, wakili wa Kelly amesitisha makala hiyo isiendelee kutumika.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club


Loading...

Toa comment