The House of Favourite Newspapers

Rugemalila, Singasinga Mambo Magumu Mahakamani (VIDEO)

0
Harbinder Singh Sethi maarufu kama ‘Singasinga’ (kulia) na mfanyabiashara James Rugemalira wakiwa kortini.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Alhamisi, Agosti 17, 2017 imeahirisha kesi inayowakabili mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder  Singh Sethi maarufu kama ‘Singasinga’ na  mfanyabiashara James Rugemalira wanaokabiliwa na mashtaka 12, yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababishia serikali hasara.

 

Kesi hiyo iliyokuwa isikilizwe na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambaye hakuwepo ilipangiwa Hakimu mwingine Cyprian Mkeha aliyeiahirisha hadi Agosti 31 mwaka huu, baada ya wakili wa serikali, kueleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika. Washitakiwa wamerudishwa rumande.

NA ABEID LIJEY | GLOBAL TV ONLINE

==========

Yaliyojiri Kesi ya Rugemalira, Singasinga Yapigwa Kalenda

Leave A Reply